Mwongozo wa chakula na ulaji Tanzania Bara
2023
Wizara ya Afya
Mwongozo wa chakula na ulaji unaofaa unatumika kama nyaraka rasmi kuongoza juu ya ulaji na mtindo bora ya maisha yenye tija katika kuboresha hali ya lishe na mtindo bora ya maisha. Pia, mwongozo huu itakuwa nyenzo muhimu katika kuwezesha masuala yanayohusu taarifa na elimu ya chakula na lishe nchini. Mwongozo huu ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuboresha hali ya lishe kwa kupitia (i) afua za lishe zinazotekelezwa na sekta mtambuka na zile zinazotekelezwa na sekta ya afya, (ii) mwongozo wa kuboresha upatikanaji wa madini na vitamini, (iii) sera inayohusu ulishaji wa watoto wachanga na wadogo, na (iv) mikakati ya kuongeza virutubisho kwenye chakula. Pia, mwongozo huu ya ulaji inasaidia utekelezaji wa mpango jumuishi wa taifa wa lishe wa pili kwa mwaka 2021-2026. Aidha,mwongozo huu unasaidia kuimarisha uhusiano wa kiuetendaji baina ya sekta za kilimo, lishe na afya katika kusimamia masuala ya lishe nchini. Mwongozo huu unakusudiwa kutumiwa na wataalam mbalimbali wakiwemo wataalamu wa lishe,watafiti , wadau wa maendeleo, waelimishaji lishe wa jamii, watumishi wa afya, walimu na wadau wengine wanaoboresha hali za lishe na afya za umma.
显示更多 [+] 显示较少 [-]